Nenda kwa yaliyomo

ISO 216

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maandishi madogo

Ugawaji wa karatasi ya ukubwa A0 hadi A9

ISO 216 ni orodha ya vipimo sanifu iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Usanifishaji (ISO) kwa ajili ya fomati za karatasi. Orodha hii inafafanua fomati za karatasi za aina "A" na "B" pamoja na A4 ambayo ni ukubwa unaotumiwa zaidi duniani. Zinatumiwa kote duniani isipokuwa Marekani bado wanatumia fomati tofauti.

Fomati zote za ISO 216 (na vipimo vya kuambatana nayo ISO 217 na ISO 269) vinafuata uhusiano wa 1: kati ya upande mrefu na upande mfupi. Faida yake ni ukikunja karatasi hizi kwa nusu yake, hata sehemu hizi zitakuwa tena na uhusiano huohuo baina ya upande ndefu na fupi. Pia eneo la kila fomati ni nusu ya eneo la fomati kubwa zaidi.

Fomati ya kimataifa ya ISO 216 inafuata utaratibu uliofafanuliwa nchini Ujerumani tangu mwaka 1922 kwa jina la DIN 476.

Vipimo vya karatasi za fomati za A na B chini ya ISO 216 na C chini ya ISO 269

[hariri | hariri chanzo]
Fomati za karatasi za ISO 216
(mm × mm)
Fomati za AFomati za BFomati za C
A0841 × 1189B01000 × 1414C0917 × 1297
A1594 × 841B1707 × 1000C1648 × 917
A2420 × 594B2500 × 707C2458 × 648
A3297 × 420B3353 × 500C3324 × 458
A4210 × 297B4250 × 353C4229 × 324
A5148 × 210B5176 × 250C5162 × 229
A6105 × 148B6125 × 176C6114 × 162
A774 × 105B788 × 125C781 × 114
A852 × 74B862 × 88C857 × 81
A937 × 52B944 × 62C940 × 57
A1026 × 37B1031 × 44C1028 × 40

    Viungo vya Nje

    [hariri | hariri chanzo]
    Wikimedia Commons ina media kuhusu: